RAIS
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema
kwamba wagombea walioenguliwa na Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi wana namna
mbili tu za kufanya ili kutafuta haki yao, moja kuomba pingamizi dhidi
yao kusikilizwa tena au kwenda Mahakama ya Usuluhishi ya Soka (CAS),
iliyo chini ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Akizungumza
na Waandishi wa Habari mchana wa leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF, Tenga amesema kwamba
TFF ilijiwekea utaratibu ambao lazima uheshimiwe.
Alisema
mchakato wa uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Februari 24, mwaka huu
ulianza vizuri na umeendelea vizuri hadi kufika hapa ulipo, ingawa
amekiri kuna matatizo.
Tenga
alisema kwamba kwa mujibu wa utaratibu wa TFF, Kamati ya Rufaa ya
Uchaguzi ndiyo chombo cha mwisho na mtu anapokwama hapo hana pa kwenda
zaidi ya CAS.
Kauli
hiyo ya Tenga imefuatia Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti
wake Iddi Mtiginjola kumuengua mgombea wa nafasi ya Urais, Jamal
Malinzi kwa madai mawili, kukosa uzoefu na kupinga waraka wa mabadiliko
ya uchaguzi.
Taarifa
ya Mtiginjola Jumatatu, ilisema kwamba mgombea pekee aliyepitishwa
katika nafasi ya Urais, inayoachwa wazi na Tenga anayeng’atuka ni
Athumani Jumanne Nyamlani.
Malinzi aliwekewa pingamizi awali, lakini akashinda mbele ya Kamati ya Uchaguzi na baadaye akakatiwa Rufaa, ambayo imemuengua.
Nyamlani
pia aliwekewa pingamizi, akashinda na akakatiwa Rufaa lakini pia
ameshinda, baada ya pingamizi alilowekewa kutupiliwa mbali.
Wengine
walioenguliwa ni Michael Wambura aliyekuwa akiwania nafasi ya Makamu wa
Rais na Ahmed Yahya aliyekuwa akiwania nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya
Ligi.
Hata hivyo, Tenga amesema kwamba tayari Malinzi na Mohamed Yahya wameomba kusikilizwa upya kwa pingamizi dhidi yao.
Kufuatia
matatizo haya, Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Jumanne wiki hii iliamua
kusimamisha kampeni za uchaguzi wa shirikisho hilo zilizopangwa kuanza
Jumatano, kuelekea uchaguzi huo Februari 24, mwaka huu.
Taarifa
ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Lyatto ilisema kwamba, Kamati yake
imechukua hatua hiyo kutokana na Mamlaka iliyonayo Kikatiba.
“1.
Kamati ya Uchaguzi, kwa mamlaka iliyonayo, kupitia Kanuni za Uchaguzi
za TFF Ibara ya 3(1), 6(1) (g) na (l), 10(5), 11(6) inayosomeka pamoja
na Ibara ya 14(1) na (2) na pia Ibara ya 26(5) na (6), imesitisha zoezi
la kampeni za uchaguzi wa TFF na TPL Board lililokuwa lianze kesho
tarehe 13/02/2013 hadi hapo itakapowatangazia, ili kuhakikisha kuwa
mchakato wa uchaguzi unakidhi kikamilifu matakwa ya Kanuni za Uchaguzi
na Katiba ya TFF,”imesema taarifa hiyo.
Aidha,
Taarifa ya Lyatto imesema; “2. Tarehe za Uchaguzi Mkuu wa TFF na TPL
Board zinabaki kama zilivyopangwa. 3. Taarifa hii inazingatia pia Ibara
ya 2(4) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF inayoagiza uongozi uliopo
madarakani kuendelea na kutekeleza majukumu ya Shirikisho hadi hapo
mchakato wa uchaguzi utakapokamilika,”.
Home
»
»Unlabelled
» TENGA AVUNJA UKIMYA SUALA LA MALINZI, AMTAKA AKWEE PIPA MPAKA FIFA
Saturday, February 16, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment