Wednesday, February 27, 2013

Na Baraka Adson

 Klabu ya Mbeya city ya jijini Mbeya imejipanga kufanya usajili wa kufa mtu ili kuhimili vishindo vya ligi kuu Tanzania bara msimu ujao wa 2013/2014 baada ya kufanikiwa kupanda kucheza ligi hiyo mwaka huu.
Kocha wa mbeya city, Juma Mwambusi (katikati) akitoa maelekezo kwa wachezaji wake kwenye moja ya mechi zake


Akizungumza na MATUKIO DUNIANI kocha mkuu wa timu hiyo Juma Mwambusi amesema klabu yao inatambua ugumu wa sasa wa ligi kuu, hivyo wanahitaji kupata wachezaji wengine wapya na wenye uzoefu ili kuungana na wale watakaobakishwa katika kikosi hicho.

"Kucheza ligi kuu si suala la kubeza, hakika ligi ni ngumu na kuna wachezaji bora, ninatakiwa kutafuta wachezaji watakaoniwezesha kuingia soka la ushindani mara nitakapoanza kuuwakilisha mkoa wa Mbeya sanjari na swahiba zetu Tanzania prisons". Mwambusi alisema.

Pia kocha huyo alitoa pongezi kubwa kwa viongozi wa jiji wakiongozwa na Mkurugenzi Jumanne Idd pamoja na mashabiki, wanachama na wadau wa soka jijini Mbeya kutoa "SAPOTI" kubwa wanapocheza ligi daraja la kwanza kwa msimu wa mwaka huu na kufanikiwa kupanda daraja kucheza ligi kuu bara msimu ujao.

"Siku zote wachezaji wanaoingia uwanjani ni kumi na mmoja, lakini mashabiki ni mchezaji wa kumi na mbili, ninawapongeza na kuwashukuru sana mashabiki na wadau wa soka jijini mbeya kutuunga mkono katika mechi zote". Mwambusi alisistiza.

Kwa upande wa ndugu zao Tanzania Prisons maarufu kama wajela jela wamewapongeza Mbeya city kwa kufanikisha lengo lao la kucheza ligi kuu bara kwa msimu ujao.

Katibu mkuu wa Prisons, Sadick Jumbe alisema ndugu zao hao kupanda ligi kuu ni hatua nzuri lakini wanapaswa kufanya usajili mzuri kutokana na ushindani uliopo ligi kuu Tanzania bara.

Pia aliwataka mashabiki wasoka jijini Mbeya kuzishangilia timu zao za mbeya zinapowajibika uwanjani na kuepukana na kasumba ya sasa ya kuishangilia mbeya city tu pindi inaposhuka dimbani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video