Wednesday, February 13, 2013


Ligu kuu Tanzania bara inaendelea leo kutimua vumbi kwenye viwanja mbalimbali.
Wakata miwa wa Kagera sugar wapo nyumbani kuvaana na wagosi wa kaya, klabu ya coastal union kutoka jijini Tanga katika uwanja wa kaitaba mkoani kagera.
Watoto wa mitaa ya kishapanda jijini Mwanza, klabu ya Toto African ni wenyeji wa polisi morogoro katika uwanja wa CCM Kirumba mwanza.
Mgambo shooting wamewakaribisha JKT Oljoro kwenye uwanja wa ccm mkwakwani mkoani Tanga.
Mtibwa sugar wapo yumbani manungu complex kuvaana maafande wa jeshi la kujenga taifa, Ruvu shooting kutoka mkoani Pwani.

YANGA inashuka uwanjani leo uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kuikabili African Lyon.
 
 Lakini  Azam inampa presha kubwa kocha Ernest Brandts ambaye ameagiza wachezaji wake kuhakikisha wanaishushia mvua ya mabao Lyon  ili kuwadhibiti wana lamba lamba hao.
 Azam iliibamiza Mtibwa Sugar  Jumapili ya wiki iliyopita mabao 4 – 1 na kukabana koo na Yanga kileleni.
 Timu zote hizo zina pointi  33, lakini Yanga inaongoza kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa wakati Simba bado inachechemea  katika nafasi ya tatu baada ya kulazimishwa sare ya bao 1 – 1 JKT Oljoro Jumamosi iliyopita jijini Arusha.
 Brandts amesema kuwa ligi sasa imefikia patamu  na hakuna kudharau timu hata moja ingawa kasi wanayokuja nayo Azam ni kubwa na inamuogopesha katika harakati zao za kutwaa ubingwa ingawa amedai kuwa  atawatuliza tu na Yanga itakuwa bingwa msimu huu.
Kocha huyo raia wa Uholanzi amewaambia wachezaji wake wajifunze kutokana na matokeo wanayopata Simba hivi sasa kwa kutambua kuwa  sasa ni muda wa kazi na  wanatakiwa kujituma zaidi ili kusaka mafanikio.
 Vita ya ubingwa  imeonekana kupamba moto katika timu tatu Yanga, Azam na Simba ingawa wekundu hao wa Msimbazi wameonekana kuchechemea katika mbio hizo.
 Ingawa Yanga inaonekana ina  ahueni zaidi katika michezo yake 11 iliyobaki kwani mechi  sita ndio zinaonekana zitaipa shida timu hiyo katika harakati zake za kuwania ubingwa wakati Azam ina mechi  saba ngumu pia wakati Simba ndio ina kazi kubwa zaidi kwani ina mechi  tisa ngumu.
 Yanga ina mechi ngumu dhidi ya  JKT Ruvu, Azam, Kagera Sugar, JKT Oljoro, Coastal Union na Simba ingawa  inapata haueni kwani mechi nyingi inacheza kwenye Uwanja wa nyumbani wakati Azam ina kazi dhidi ya  JKT Ruvu, Yanga,  Ruvu Shooting, Simba, Coastal na Oljoro na Mgambo Shooting.
 Simba yenyewe itabidi ifanye kazi ya ziada  kuziadabisha  Prisons, Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar, Coastal Union, Kagera, Azam, Toto, Mgambo Shooting  na Yanga.

MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
YANGA
15
10
3
2
17
33
2
AZAM FC
16
10
3
3
13
33
3
SIMBA
16
7
7
2
11
28
4
COASTAL
16
7
6
3
4
27
5
RUVU SHOOTING
15
7
3
5
3
24
6
KAGERA
16
6
6
4
2
24
7
MTIBWA
16
6
5
5
2
23
8
JKT OLJORO
16
5
6
5
1
21
9
MGAMBO
16
5
3
7
-6
18
10
PRISONS
16
4
6
6
-6
17
11
JKT RUVU
15
4
4
7
-8
16
12
TOTO
16
2
7
7
-9
13
13
POLISI
15
2
4
9
-10
10
14
LYON
16
2
3
10
-16
9


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video