Tuesday, February 12, 2013

>>ALIJIUZULU MARA BAADA YA NIGERIA KUTWAA UBINGWA AFRIKA!!
>>KESHI & EL GOHARY NDIO PEKEE MABINGWA AFRIKA KAMA WACHEZAJI NA MAKOCHA!
STEPHEN_KESHIStephen Keshi atabakia kama Kocha wa Mabingwa wapya wa Afrika, Nigeria, kufuatia kuingilia kati kwa Waziri wa Michezo wa Nchi hiyo, Bolaji Abdillahi, aliemshawishi afute msimamo wake wa kujiuzulu alioutoa mara baada ya kufanikisha Nchi yake kutwaa Ubingwa wa AFCON 2013 Jumapili huko Afrika Kusini kufuatia mgogoro wake na Shirikisho la Soka, NFF.
Jumatatu, Keshi alitangaza kujiuzulu wakati akiongea kwenye Kituo cha Redio cha Afrika Kusini, Metro FM.
Lakini Waziri wa Michezo wa Nigeria , ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Kitaifa ya Michezo ya Nigeria, aliingilia kati na kumshawishi Keshi, mwenye Miaka 51, afute uamuzi huo walipokutana Jumatatu huko Johannesburg, Afrika Kusini.
Keshi aliafikiana na Waziri wa Michezo, Bolaji Abdillahi, na sasa ataendelea kuwa Kocha wa Nigeria.
Pia, imebainishwa kuwa Kikao cha kusaka muafaka kati ya Keshi na NFF kitafanyika huko Abuja mara baada ya Mabingwa hao kutua huko Abuja ambako watapokelewa kwa shangwe na Wanigeria na kukaribishwa Ikulu kukutana na Rais wa Nigeria.
Jumapili iliyopita, kwenye Uwanja wa FNB, Soccer City, Soweto, Johannesburg, Nigeria walitwaa Kombe la Ubingwa wa Afrika walipoichapa Burkina Faso Bao 1-0 na hii ni mara yao ya 3 kuwa Mabingwa baada ya kushinda Mwaka 1980 na 1994.
Stephen Keshi ni Mtu pekee, baada ya Mahmoud El Gohary wa Egypt, kuweza kutwaa Ubingwa wa Afrika kama Mchezaji na Kocha wa Nchi yake.

SOKA IN BONGO

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video