wachezaji wa yanga wakishangila moja ya mabao waliyowahi kufunga siku za nyuma |
Mabingwa Afrika Mashariki na kati ,Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam
,wanataraji kushuka ugani katika katika mechi ya kimataifa ya kirafiki
dhidi ya Black Leopards ya Afrika Kusini.
Kocha mkuu wa timu hiyo Ernie Brandts amesema kuwa kikosi chake kipo
fiti kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya kandanda Tanzania
bara.
Kocha huyo amesema kuwa anaamini vijana wake wamejinoa vilivyo
walipokuwa Uturuki huku akitaraji kufanya vizuri katika mechi ya
kimataifa ya kirafiki dhidi ya Black Leopards.
Black Leopards ambayo inashiriki ligi kuu Afrika Kusini ikiwa nafasi
ya 12 katika ligi kuu nchini humo maarufu kama PSL ambayo
inashirikisha timu 16.Timu hiyo inataraji kuwasili hapa nchini
Alhamisi wiki hii.
Akizungumzia mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara,kocha Brandts
amessema kuwa anataraji kupata upinzani wa hali ya juu kutokana na
timu TANO za juu kujiimarisha zaidi kwa maandalizi kamambe.
Licha ya kutoshinda mechi katika ziara ya timu yake nchini Uturuki
kocha Brandts amesema kuwa vijana wake watakuwa wamepata uzoefu wa
mechi za kimataifa ambapo walicheza mechi tatu nay a wikiendi hii
dhidi ya Black Leopards itakuwa mechi ya NNE.
Kwa mujibu wa waratibu wa mechi ya Yanga na Black Leopards kampuni ya
Prime Time Promotion wametangaza kiingilio kuwa kati ya shilingi ELFU
TANO na ELFU THELATHINI.
Katika hatua nyingine klabu hiyo inataraji kufanya mkutano mkuu
Jumapili wiki hii ambao utafanyika katika ukumbi wa Police Officers
Mess jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment