Balozi wa marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt amekabidhi jumla ya dola za
kimarekani 97,635 sawa na shilingi za kitanzania milioni 151 ikiwa ni ruzuku kwa
mashirika 11 yanayojishugulisha na maendeleo ya jamii nchini.
Balozi huyo wa marekani amesema ruzuku hizo
zinalenga kusaidia sekta ya elimu,
maendeleo ya kiuchumi, maji , nishati ya umeme wa jua , wakimbizi na ugonjwa la
ukimwi.
Balozi wa Marekani Tanzania, Alfonso Lenhardt |
Mikoa iliyonufaika na ruzuku hizo ni pamoja na
Arusha, Geita, kagera, mbeya, mara, njombe na morogoro.
Fedha hizo zimetolewa kupitia Mfuko wa balozi wa
kusaidia miradi ya kujitegemea ya jamii ulioanzishwa wakati wa Muhula wa kwanza
wa utawala wa mwal JK nyerere
Kwa miaka 47 mfuko huo umesaidia taasisi na
vikundi vya kijamii kutoka kila mkoa wa
Tanzania kuboresha maisha ya watanzania huku kipaumbele kikiwa katika
kutokomeza ugonjwa wa ukimwi katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi.
0 comments:
Post a Comment