Jeshi la polisi kanda Maalum Dar es Salaam
limewataka wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM kutulia wakati madai
yao ya kuhitaji ulinzi wao na mali zao kufuatia matukio ya
kuporwa,kupigwa,kulawitiwa na kubakwa.
Hata hivyo kamanda wa kanda Maalum Dar es Salaam
Suleimani Kova amesema atayashughulikiwa madai hayo baada aya kuzungumza na
wanafunzi na wananchi wa kigamboni mazungumzo yaliyofanyika katika uwanja wa
Machava Kigamboni.
MATUKIO KATIKA PICHA YA MAANDAMANO YA IFM
|
wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa
fedha IFM wakiwa wamejazana kwenye kivuko huku wakigoma kushuka hata baada ya
kuamriwa kwamba kiusalama itakuwa vigumu kwao kusafiria kwenda kigamboni. |
|
Hatimaye wanafunzi wa IFM wamekubali kushuka
na kupungua ili kuwapisha wengine na kuvuka kwa awamu kuelekea kigamboni |
|
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia
akiwaagiza wanafunzi wa chuo cha uongozi wa fedha IFM kuelekea eneo la uwanja
wa Machava kwa ajili ya majadiliano lakini wanafunzi hao wakakataa na kuanza
kuongea maneno ya kashfa ndipo mabomu ya machozi yakawatawanya wanafunzi hao.
|
|
Baada ya mabomu ya machozi wanafunzi
wanajisalimisha kwa kunyoosha mikono juu.
|
|
wanafunzi wakiruka kichura huku wengine
wakitembelea magoti |
|
wakipakiwa katika gari ya polisi
kuelekea kituo cha polisi Kigamboni |
|
Pata shika nguo kuchanika hapa
wanaonekana Wanafunzi wa IFM wakigombea wenyewe kuingia kwenye gari dogo la
Polisi kuelekea kituo cha Polisi Kigamboni. |
|
Mwanafunzi wa kike ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiwa
ameanguka kufuatia kashkash baina ya jeshi la polisi na wanafunzi wa IFM |
|
Mwanafunzi mwingine wa kike akisaidiwa
kuinuka baada ya kuanguka katika purukushani hizo. |
0 comments:
Post a Comment