Upungufu wa walimu umeelezwa kuwa ni moja ya
sababu zinazochangia matokeo yasiyoridhisha katika shule ya msingi Mabwepande
iliyoko katika manispaa ya Kinondoni
WANAFUNZI WAKIWA DARASANI KUMSIKILIZA MWALIMU WAO |
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Davis Mkaruka amesema idadi ya walimu waliopo
shuleni hapo haitoshelezi mahitaji halisi ya wanafunzi
Amesema shule hiyo ina jumla ya walimu 15 huku
ikiwa na wanafunzi zaidi ya elfu moja
Mwalimu mkuu huyo amesema katika matokeo ya
mtihani wa darasa la saba mwaka jana wanafunzi 30 kati ya 94 ndio waliofaulu
mtihani,matokeo ambayo amesema bado hayaridhishi
Ameiomba idara ya elimu katika manispaa ya
Kinondoni kuongeza idadi ya walimu pamoja na kutoa mafunzo ya mara kwa mara ili
walimu waweze kumudu mabadiliko ya mitaala
0 comments:
Post a Comment