Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeahirisha
uchaguzi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA)
uliokuwa ufanyike leo (Januari 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Uchaguzi
umeahirishwa kwa vile ulitaka kufanyika bila kuzingatia Katiba ya TAFCA
Ibara ya 32(1) na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF Ibara ya 10(6)
na 26(2), hivyo Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeahirisha uchaguzi huo kwa
vile nafasi zilizoombwa kugombewa na idadi ya waombaji uongozi haikidhi
matakwa ya Katiba ya TAFCA.
Pia
taratibu za kikanuni ikiwa ni pamoja na kuwaarifu waombaji uongozi
ambao hawakukidhi matakwa ya Katiba ya TAFCA hazikukamilika kwa mujibu
wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Licha
ya upungufu huo, TAFCA haikuwasilisha taarifa za mchakato mzima kama
ilivyoombwa na TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya
Uchaguzi ya TAFCA kuandaa uchaguzi mpya utakaokidhi matakwa ya Kamati ya
TAFCA baada ya Uchaguzi Mkuu wa TFF.
TFF
inaishauri TAFCA kutumia fursa ya Mkutano Mkuu wa leo (Januari 19 mwaka
huu) kujadili mustakabali wa TAFCA kwa kuwa chama hicho kimeshindwa
mara mbili kupata idadi ya wagombea wanaokidhi akidi ya Kamati ya
Utendaji.
Pia TAFCA haijawahi kufanya mikutano ya Kamati ya Utendaji na Mkutano Mkuu kwa karibu miaka minne.
0 comments:
Post a Comment