Okwi |
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans
Poppe amesema
kwamba, Okwi amekamilisha vipimo na kila
kitu na tayari amesaini mkataba.
“Tunasubiri kulipwa fedha zetu tu, viongozi watakwenda
Tunisia kuchukua fedha za mauzo ya mchezaji huyo,”alisema Poppe.
Okwi amekuwa akipiga chenga kuripoti kambini Simba SC na
alikuwa hata hapokei simu za viongozi wa klabu hiyo kila alipopigiwa.
Kufuatia hatua hiyo, uongozi ulimuengua kwenye programu ya
safari ya Oman na sasa inabainika ametua Sahel.
Okwi, aliyezaliwa Desemba 25, mwaka 1992 aliisajiliwa Simba
akitoea SC Villa ya Uganda mwaka 2010 akiwa kinda wa miaka 17, akisajiliwa kwa
dau la dola za Kimarekani 40,000.
Baada ya kumaliza mkataba wake wa awali, Desemba mwaka jana
aliongeza mkataba wa miaka miwili na Simba SC ambao kabla hajaanza kuutumikia,
anahamia Sahel.
0 comments:
Post a Comment