Kiungo
wa Manchester United Darren Fletcher ataukosa Msimu huu uliobakia baada
ya kwenda kufanyiwa Operesheni ili kutibu ugonjwa sugu wa Tumbo
uliokuwa ukimsibu kwa muda mrefu na kumfanya awe nje ya Uwanja kwa Miezi
11 kuanzia Desemba 2011 na kurejea tena mwanzoni mwa Msimu huu.
Msimu huu alicheza Jumla ya Mechi 13 kwa
Manchester United na Nchi yake Scotland na Mechi yake ya mwisho ilikuwa
ni kuingizwa kutokea Benchi katika Dakika ya 89 Manchester United
walipoifunga Newcastle 4-3 hapo Desemba 26, 2012.
++++++++++++++++++++++++
WASIFU wa FLETCHER:
-UMRI: 28
-MECHI MAN UNITED: 310 MAGOLI: 23
-MECHI SCOTLAND: 61 MAGOLI: 7
-MATAJI: 4 UBINGWA LIGI
KUU (2007, 2008, 2009, 2011), 1 FA CUP (2004), 2 LIGI CUP (2006, 2010),
1 CHAMPIONS LEAGUE (2008), 1 WORLD CLUB CUP (2008)
-MECHI ya KWANZA: Man United v BASEL, 12 Machi 2003 (UEFA Champions League)
-MECHI ya MWISHO: Man United v NEWCASTLE, 26 Desemba 2012 (Barclays Premier League)
++++++++++++++++++++++++
Klabu ya Manchester United imethibitisha habari hizi na kusema Opersheni hiyo ilikuwa imepangwa.
Akizungumzia habari hizi, Meneja mpya wa
Scotland, Gordon Strachan, amemtakia kila heri Darren Fletcher, ambae
ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya Scotland, na pia kusisitiza Fletcher
atabaki kama Nahodha na yupo kwenye mipango yake ya baadae.
Fletcher anao Mkataba na Manchester United hadi Mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment