COPA del REY: KESHO ni BARCA v MALAGA!
LEO, Mabingwa wa Spain, Real Madrid,
ambao Msimu huu matumaini yao makubwa kutwaa Taji huko Spain yamebaki
kwenye COPA del REY, watatinga Uwanjani kwao Santiago Bernabeu kucheza
na Valencia katika Mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya Kombe hilo na huko
Italy, pia kutakuwa na Robo Fainali ya COPPA ITALIA kati ya Inter Milan
na Bologna.
Real Madrid, baada ya kucheza bila
Supastaa wao Cristiano Ronaldo katika Mechi yao ya mwisho ya La Liga
hivi juzi na kutoka 0-0 na Timu goigoi Osasuna kwa vile alikuwa
Kifungoni kwa Mechi moja, leo Nyota huyo atatinga dimbani.
Huko Italy, washiriki wa Nusu Fainali ya kwanza washajulikana wakati Juventus watakapoivaa Lazio hapo Januari 22.
Mshindi kati ya Inter Milan na Bologna
na yule wa Mechi kati ya Fiorentina na AS Roma ndio watacheza kwenye
Nusu Fainali ya pili.
Huko Spain, Robo Fainali nyingine za Copa del Rey zitakuwa Jumatano Januari 16, Mechi mbili, na Ijumaa Mechi moja.
Mabingwa watetezi wa COPA del Rey, Barcelona, wao watacheza Jumatano na Malaga Uwanjani Nou Camp.
...................................................
ROBO FAINALI
Jumanne Januari 15
[SAA 5 Usiku]
Real Madrid CF v Valencia
Jumatano Januari 16
[SAA 3 na Nusu Usiku]
Real Zaragoza v Sevilla FC
[SAA 5 na Nusu Usiku]
Barcelona v Malaga
Ijumaa Januari 18
[SAA 6 Usiku]
Atletico Madrid v Real Betis
Jumatano Januari 23
Marudiano
Sevilla FC v Real Zaragoza
Valencia v Real Madrid CF
Malaga v Barcelona
Real Betis v Atletico Madrid
++++++++++++++++++++++
COPPA ITALIA
ROBO FAINALI
RATIBA:
Jumanne Januari 15
[SAA 5 Usiku]
Inter Milan v Bologna
Jumatano Januari 16
[SAA 5 Usiku]
Fiorentina v AS Roma
NUSU FAINALI:
Jumanne Januari 22
SS Lazio v Juventus
Jumanne Januari 29
Juventus v SS Lazio
0 comments:
Post a Comment