Saturday, January 19, 2013

kutoka blog ya soka In Bongo


BPL_LOGOBPL, Barclays Premier League, itakuwa na Mechi 7 Jumamosi, mbili Jumapili, ni SUPER SUNDAY kwa kuwa na BIGI MECHI Chelsea v Arsenal na Tottenham v Man United, na Jumatatu ipo Mechi moja.
ZIFUATAZO NI RATIBA, HALI ZA WACHEZAJI NA VIKOSI VYA KILA TIMU PAMOJA NA MAREFA WA MECHI HIZO:
+++++++++++++++++++++++
BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:  
Jumamosi Januari 19
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Norwich
Man City v Fulham
Newcastle v Reading
Swansea v Stoke
West Ham v QPR
Wigan v Sunderland
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Brom v Aston Villa
Jumapili Januari 20
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea v Arsenal
[SAA 1 Usiku]
Tottenham v Man United
Jumatatu Januari 21
[SAA 5 Usiku]
Southampton v Everton
+++++++++++++++++++++++
Jumamosi Januari 19
LIVERPOOL v NORWICH
Straika mpya wa Liverpool Daniel Sturridge, baada ya kufunga Bao mbili katika Mechi zake mbili za kwanza, anasaka Mechi yake ya kwanza kuanza tangu mwanzo badala ya kuanzia Benchi.
Beki wa Liverpool Jose Enrique bado ni majeruhi hivyo Glen Johnson ataendelea kucheza kama Fulbeki wa kushoto.
Norwich itawakaribisha tena majeruhi wao waliopona Jonny Howson, Andrew Surman na Grant Holt baada ya Meneja wao Chris Hughton kuthibitisha kupona kwao.
Lakini Norwich itaendelea kuwakosa majeruhi Steven Whittaker na Steve Morison.
VIKOSI:
Liverpool: Reina, Wisdom, Agger, Skrtel, Johnson, Gerrard, Lucas, Henderson, Sterling, Sturridge, Suarez, Jones, Carragher, Coates, Robinson, Shelvey, Suso, Downing, Borini. 
Norwich City: Bunn, R Martin, Bassong, Barnett, Garrido, Howson, Snodgrass, Johnson, E Bennett, Kane, Surman, Turner, Jackson, Pilkington, Hoolahan, Fox, Tierney, Tettey, R Bennett, Lappin, Smith, Rudd, Steering.
Refa: Michael Oliver 
MANCHESTER CITY v FULHAM
Manchester City itakuwa nao tena majeruhi wao waliopona Sergio Aguero na Jack Rodwell na pia Samir Nasri atarejea baada ya kumaliza Kifungo chake.
Man City itawakosa Wachezaji Yaya Toure, Kolo Toure na Abdul Razak ambao wako na Nchi yao Ivory Coast kwa ajili ya AFCON 2013 na pia majeruhi Micah Richards na Maicon.
Fulham itawakosa majeruhi Mahamadou Diarra (Goti) na Kerim Frei (Nyonga).
VIKOSI:
Man City: Hart, Pantilimon, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov, Clichy, Rekik, Milner, Silva, Barry, Garcia, Sinclair, Rodwell, Nasri, Aguero, Tevez, Dzeko, Balotelli. 
Fulham: Schwarzer, Stockdale, Somogyi, Etheridge, Riether, Hangeland, Hughes, Senderos, Riise, Briggs, Dejagah, Baird, Sidwell, Karagounis, Kacaniklic, Duff, Richardson, Kasami, Ruiz, Rodallega, Berbatov, Petric, Davies.
Refa: Jon Moss 
NEWCASTLE v READING
Meneja wa NewcastleAlan Pardew kuwepo tena Beki Steven Taylor aliepona maumivu na Shola Ameobi aliemaliza Kifungo chake.
Kiungo wa Newcastle Hatem Ben Arfa bado ni majeruhi.
Reading wanaweza kuwachezesha Wachezaji wao wapya Stephen Kelly na Hope Akpan lakini itawakosa majeruhi Jason Roberts (Paja) na Kipa Alex McCarthy (Bega) ingawa Mikele Leigertwood inasemekana amepona maumivu yake.
VIKOSI:
Newcastle: Krul, Elliot, Tavernier, Perch, Williamson, Coloccini, Debuchy, Santon, Gutierrez, Anita, Cabaye, Cisse, Bigirimana, Obertan, Sammy Ameobi, Amalfitano, Marveaux, Abeid, Ranger, Ferguson, Shola Ameobi, Taylor.
Reading: Federici, Ugwu, Taylor, Gunter, Kelly, Cummings, Pearce, Morrison, Mariappa, Shorey, Harte, McAnuff, Carrico, Akpan, Tabb, Karacan, Kebe, McCleary, Robson-Kanu, Leigertwood, Le Fondre, Hunt, Pogrebnyak
Refa: Andrew Marriner 
SWANSEA v STOKE
Beki wa Stoke Andy Wilkinson huenda asicheze baada ya kuumia kwenye Mechi iliyopita lakini mwenzake Ryan Shotton amepona na pia Kipa Asmir Begovic na Kiungo Charlie Adam wanaweza kucheza baada ya kupumzishwa Mechi iliyopita.
Swansea watamkosa Kiungo Kemy Agustien anaeuguza enka lakini huenda wakampa namba Mchezaji wao mpya wa Mkopo Roland Lamah alietokea Osasuna.
VIKOSI:
Stoke: Begovic, Shotton, Shawcross, Cameron, Huth, Upson, Wilkinson, Whelan, Nzonzi, Walters, Kightly, Etherington, Jones, Sorensen, Whitehead, Crouch, Jerome, Adam, Palacios, Owen.
Swansea: Vorm, Bartley, Flores, Williams, Britton, Lita, Michu, Graham, Hernandez, Dyer, Lamah, Routledge, Monk, Shechter, Moore, De Guzman, Tiendalli, Rangel, Ki, Tremmel, Gower, Richards, Davies.
Refa: Mike Dean 
WEST HAM v QPR
West Ham watakuwa nae tena Beki Joey O'Brien na pia huenda Sentahafu James Collins akawa fiti baada ya kuikosa Mechi na Man United hivi juzi.
Wengine wanaoweza kucheza ni Mark Noble na Joe Cole baada ya kupumzishwa Mechi iliyopita na Manchester United na pia Mchezaji mpya Wellington Paulista huenda akacheza sehemu ya Mechi.
West Ham itawakosa Modibo Maiga ambae yuko na Nchi yake Mali kwenye AFCON 2013 na majeruhi Andy Carroll na George McCartney.
QPR inaweza ikamchezesha Mchezaji wao mpya kutoka France Loic Remy na pia majeruhi aliepona Junior Hoilett lakini majeruhi watakaokosekana ni Esteban Granero na Armand Traore.
Wengine ambao hawatacheza ni Samba Diakite ambae yuko AFCON 2013 na majeruhi Jose Bosingwa, Andrew Johnson na Bobby Zamora.
VIKOSI:
QPR: Green, Cesar, Murphy, Cerny, Onuoha, Hill, Nelsen, Ben-Haim, Ferdinand, Mbia, Hoilett, Park, Fabio, Derry, Taarabt, Faurlin, Wright-Phillips, Ephraim, Mackie, Cisse, Campbell, Remy. 
West Ham squad: Jaaskelainen, Demel, Potts, Reid, Collins, Tomkins, Jarvis, J Cole, Noble, Collison, Vaz Te, Nolan, Diarra, C Cole, Chamakh, O'Brien, O'Neil, Taylor, Diame, Spiegel.
Refa: Howard Webb 
WIGAN v SUNDERLAND
Majeruhi wa Wigan ni Antolin Alcaraz, Ivan Ramis, Adrian Lopez, Ben Watson, Albert Crusat na Ryo Miyaichi.
Wachezaji wapya wa Wigan, Roger Espinoza na Angelo Henriquez, huenda wakacheza.
Baada ya Bosi wa Sunderland Martin O'Neill kuwapumzisha John O'Shea na Steven Fletcher katika Mechi iliyopita huenda Wachezaji hao wakacheza Mechi hii pamoja na wapya Beki Kader Mangane na Kiungo Alfred N'Diaye lakini Nahodha wao Lee Cattermole huenda asicheze kwa vile amejitonesha Goti baada ya kupona na kurudi Uwanjani Mechi iliyopita.
VIKOSI:
Wigan: Al Habsi, Pollitt, Boyce, Caldwell, Figueroa, Beausejour, Gomez, Jones, Maloney, Espinoza, McCarthy, McArthur, Stam, McManaman, Di Santo, Henriquez, Boselli, Fyvie, Redmond, Mustoe, Golobart. 
Sunderland: Mignolet, Westwood, Bardsley, O'Shea, Kilgallon, Bramble, Mangane, N'Diaye, Gardner, Colback, McClean, Larsson, Johnson, Vaughan, Sessegnon, Fletcher, Saha, Campbell, Wickham, McFadden.
Refa: Anthony Taylor 
WEST BROM v ASTON VILLA
Bosi wa West Brom Steve Clarke anangoja Ripoti ya Madaktari ya Dakika za mwisho ili kupata uhakika kama majeruhi wake watatu wanaweza kucheza Mechi hii.
Majeruhi hao ni Kiungo Claudio Yacob, na Mastraika  Shane Long na Marc-Antoine Fortune.
Nahodha wa Aston Villa Ron Vlaar, baada ya kuwa nje kwa Wiki 7, yupo tena Kikosini lakini Winga Marc Albreighton na Beki Chris Herd hawamo kwa kuwa ni majeruhi.
VIKOSI:
West Brom: Foster, Myhill, Daniels, Jones, Olsson, McAuley, Tamas, Dawson, Popov, Ridgewell, Dorrans, Yacob, Thorne, Brunt, Morrison, Thomas, Odemwingie, Long, Lukaku, Fortune, Rosenberg, El Ghanassy, Nabi
Aston Villa: Guzan, Marshall, Lowton, Vlaar, Clark, Lichaj, Stevens, Bennett, Ireland, N'Zogbia, Bannan, Delph, Holman, Westwood, Benteke, Agbonlahor, Bent, Bowery, Weimann, Burke, Johnson, Williams, Carruthers.
Refa: Lee Probert 
Jumapili Januari 20 
CHELSEA v ARSENAL 
Sentahafu wa Arsenal Laurent Koscielny amemaliza Kifungo chake cha Mechi moja lakini Kiungo Mikel Arteta na Tomas Rosicky ni majeruhi na Straika Gervinho yuko AFCON 2013 na Nchi yake Ivory Coast.
Chelsea huenda wakamwanzisha Nahodha wao John Terry ambae aliumia tangu Novemba lakini juzi alitokea Benchi kwenye Mechi na Stoke City ya FA CUP.
Lakini Chelsea itawakosa Wanigeria John Obi Mikel na Victor Moses ambao wako AFCON 2013 na Nchi yao pamoja na majeruhi wa muda mrefu Oriol Romeu.
VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Gibbs, Vermaelen, Mertesacker, Sagna, Cazorla, Diaby, Coquelin, Walcott, Wilshere, Giroud, Mannone, Koscielny, Ramsey, Podolski, Oxlade-Chamberlain, Santos, Arshavin, Jenkinson.
Chelsea: Cech, Turnbull, Azpilicueta, Ferreira, Ivanovic, Luiz, Cahill, Terry, Cole, Bertrand, Lampard, Ramires, Mata, Oscar, Hazard, Marin, Torres, Ba, Ake
Refa: Martin Atkinson
TOTTENHAM v MANCHESTER UNITED
Kiungo wa Tottenham Scott Parker huenda akaanza Mechi yake ya kwanza tangu Aprili hasa baada ya Kiungo wa Brazil Sandro kuumia Goti ambalo litamweka nje Msimu wote uliobakia.
Tottenham pia itacheza bila ya Straika wao Striker Emmanuel Adebayor ambae yuko AFCON 2013 na Nchi yake Togo na pia itawakosa majeruhi William Gallas na Younes Kaboul.
Majeruhi pekee wa Man United ni Jonny Evans anaeuguza Musuli za Pajani na Darren Fletcher ambae ni mgonjwa na atakosekana Msimu wote uliobaki.
VIKOSI:
Tottenham: Lloris, Friedel, Gomes, Walker, Naughton, Dawson, Vertonghen, Caulker, Assou-Ekotto, Lennon, Sigurdsson, Falque, Townsend, Livermore, Dempsey, Carroll, Mason, Huddlestone, Parker, Dembele, Bale, Defoe.
Manchester United: Lindegaard, De Gea, Amos, Smalling, Vidic, Ferdinand Evans, Buttner, Evra, Cleverley, Giggs, Fletcher, Anderson, Scholes, Carrick, Kagawa, Nani, Hernandez, Rooney, Welbeck, Van Persie.
Refa: Chris Foy
Jumatatu Januari 21 
SOUTHAMPTON v EVERTON
Baada ya kuzikosa Mechi mbili, Beki wa Evarton Johnny Heitinga huenda akacheza lakini Fulbeki Tony Hibbert na Kiungo Darron Gibson bado ni majeruhi.
Southampton itatinga Mechi hii wakiwa na Meneja mpya Mauricio Pochettino kutoka Argentina baada ya kumtimua Nigel Adkins.
Majeruhi pekee wa Southampton ni Adam Lallana ambae, hata hivyo, ameshaanza tena mazoezi.
VIKOSI:
Everton: Howard, Jagielka, Distin, Heitinga, Baines, Oviedo, Naismith, Hitzlsperger, Osman, Pienaar, Fellaini, Jelavic, Mucha, Duffy, Neville, Anichebe, Vellios, Gueye, Coleman.
Southampton: K Davis, Gazzaniga, Boruc, Clyne, Richardson, Stephens, Fox, Shaw, Yoshida, Hooiveld, Martin, Reeves, Ward-Prowse, Do Prado, Cork, Chaplow, De Ridder, Ramirez, Schneiderlin, S Davis, Puncheon, Lee, Lambert, Rodriguez, Lallana.
Refa: Neil Swarbrick
 

Liverpool kumsaini Mbrazil, Zaha Jumatatu ni Man au Arsenal, Big Sam kwa Pilato!!

Jumamosi, 19 Januari 2013 10:56
Chapisha Toleo la kuchapisha
SAM_ALLARDYCEKlabu ya Liverpool iko mbioni kumsaini Chipukizi wa Barazil Philippe Coutinho huku hatima ya Kinda wa Crystal Palace, Wilfried Zaha, kujulikana Jumatatu na Meneja wa West Ham, Sam Allardyce, amefunguliwa mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa kukiuka Kanuni kufuatia kauli yake dhidi ya Refa aliechezesha Mechi yao na Manchester United.
Liverpool na Mbrazil
Liverpool wako mbioni kusaini Mchezaji wao wa Pili katika Dirisha hili la Uhamisho la Mwezi Januari baada ya kutoa Ofa ya Pauni Milioni 8 kumchukua Kiungo wa Inter Milan Philippe Coutinho.
Coutinho, Miaka 20, ambae ameichezea Brazil mara moja na alichukuliwa na Inter Milan akiwa na Miaka 16 tu na kubaki kwao Brazil kwa Mkopo hadi 2010 ambako ndio alitua Inter Milan na kucheza Mechi 28 lakini Msimu uliopita alipelekwa Spain kuchezea Espanyol kwa Mkopo.
Mchezaji mwingine alienunuliwa na Liverpool hii Januari ni Straika kutoka Chelsea Daniel Sturridge aliechukuliwa kwa Dau la Pauni Milioni 12.
Zaha
Crystal Palace > Arsenal au Man United
Habari za ndani zimedokeza kuwa Uhamisho wa Wilfried Zaha wa Crystal Palace kwenda Manchester United au Arsenal utajulikana mwanzoni mwa Wiki ijayo.
Ingawa Man United ndio inayopewa nafasi kubwa kumchukua Kinda huyo, hasa baada ya Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, David Gill, kukiri kuwa wamekuwa wakimfuatilia, lakini pia Arsenal wamekuwa wakimwinda.
Hata akiuzwa kwa sasa, Crystal Palace imekuwa ikisisitiza kipengele cha kubaki na Mchezaji huyo hadi mwishoni mwa Msimu ili awasaidie kuwapandisha Daraja.
Frazier
Sunderland > Cardiff City
Fraizer Campbell yupo mbioni kukamilisha Uhamisho wa £600,000 kutoka Sunderland kwenda Cardiff City.
Straika huyo wa zamani wa Manchester United ambae ameichezea England mara moja amekuwa akiandamwa na tatizo la Goti baada ya kuumia vibaya mara mbili katika Goti hilo hilo moja ambalo limemfanya kiwango kushuka.
Meneja wa Sunderland, Martin O'Neill, anategemewa kumnunua Danny Graham kutoka Swansea kwa Pauni Milioni 5 ili kumbadili Frazier Campbell.
M'Vila 
Rennes > QPR
Kiungo huyo wa Klabu ya Rennes ya France ambae anathaminiwa kwa Pauni Milioni 7 anawindwa na Meneja wa QPR Harry Redknapp lakini pia zipo Klabu nyingine zinazomwandama.
Akiongea kuhusu Yann M'Vila, Loïc Rémy amesema: "Ningependa aje QPR tuwe pamoja. Nishamwambia hapa ni pazuri."
Sam Allardyce ashitakiwa na FA
Meneja wa West Ham Sam Allardyce amefunguliwa Mashitaka ya Utovu wa Nidhamu na FA, Chama cha Soka England, kufuatia kauli yake mara baada ya Timu yake Jumatano iliyopita kufungwa Bao 1-0 na Manchester United na kutupwa nje ya FA CUP.
Alardyce alidai uamuzi wa kuwanyima Penati Uwanjani Old Trafford na kuwapa Man United Penati ni sababu ya kucheza Uwanja wa Nyumbani.
Hata hivyo Penati waliyopewa Man United ilipaishwa na Straika Wayne Rooney. Allardyce amepewa hadi Januari 23 kujibu Mashitaka hayo.
Penati ambayo West Ham wanaidai ni pale Fulbeki Rafael alipokontroli mpira na Paja na kisha kumgonga Mkononi.
Allardyce alikaririwa akisema: “Unaona kila mara Old Trafford! Hamna tofauti kati ya kushika kwa Rafael na Jordan Spence. Ila Spence anachezea West Ham, Timu ya ugenini na Rafael ni Mchezaji wa nyumbani Old Trafford.”
Taarifa ya FA imesema: “Shitaka hili linahusiana na kuvunjwa kwa Kanuni ya FA E3.”

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video