Saturday, January 19, 2013

45 WAOMBA KUWANIA UONGOZI TFF
Wanamichezo 45 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Februari 24 mwaka huu. Nafasi zinazowaniwa ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha kanda 13 tofauti.

Waombaji wapya 11 waliojitokeza leo (Januari 18 mwaka huu) ni Richard Rukambura anayeomba urais wakati kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kaliro Samson, Jumbe Magati, Richard Rukambura, Omari Walii, Ahmed Mgoyi, John Kiteve, Stanley Lugenge, Francis Ndulane, Riziki Majara na Hassan Othuman Hassanoo.

Mwisho wa kuchukua fomu kwa waombaji wote ni leo (Januari 18 mwaka huu) saa 10 kamili alasiri. Fomu pia zinaweza kuchukuliwa katika tovuti ya TFF ambayo ni www.tff.or.tz na kurejeshwa kupitia email ya [email protected] Pia Kanuni za Uchaguzi za TFF zinapatikana katika tovuti hiyo.

Orodha kamili ya waombaji ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura (Rais). Walioomba kuwania nafasi ya Makamu wa Rais ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia.

Kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Salum Chama na Kaliro Samson (Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).

Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na Ruvuma).

Athuman Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Nyange, Hassan Othman Hassanoo, Riziki Majara na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala, Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).

WATATU ZAIDI WAOMBA UONGOZI BODI YA LIGI KUU
Waombaji watatu wapya wamejitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ambayo uchaguzi wake utafanyika Februari 22 mwaka huu.

Walioingia leo (Januari 18 mwaka huu) kwenye kinyang’anyiro hicho ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar anayeomba uenyekiti wakati Christopher Peter wa Moro United na Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza wanaoomba ujumbe wa Bodi kuwakilisha klabu za Ligi Daraja la Kwanza.

Orodha kamili ya waombaji uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuf Manji wa Yanga wanaoomba uenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa Azam.

Kwa upande wa wajumbe wawili kuwakilisha klabu za Daraja la Kwanza ni  Christopher Peter Lunkombe wa Moro United ya Dar es Salaam na Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza.

RWIZA, LIUNDA KUSIMAMIA MECHI ZA CAF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewateua Watanzania Leslie Liunda na Alfred Rwiza kuwa makamishna wa mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika zinazoanza mwezi ujao.

Rwiza ameteuliwa kuwa kamishna wa mechi kati ya APR ya Rwanda na Vital’O ya Burundi itakayochezwa nchini Rwanda kati ya Februari 15 na 17 mwaka huu.

Naye Liunda atakuwa kamishna wa mechi ya marudiano kati ya Tusker ya Kenya na St. Michel United ya Seychelles itakayochezwa Kenya kati ya Machi 1 na 3 mwaka huu. Mechi zote ni za raundi ya awali.

WATANZANIA KUZICHEZESHA URA, COTTON SPORT
Waamuzi wanne wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuchezesha mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa kati ya URA ya Uganda na Cotton Sport ya Cameroon itakayochezwa jijini Kampala kati ya Machi 1 na 3 mwaka huu.
 
Orden Mbaga ndiye atakayekuwa mwamuzi wa kati na atasaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Jesse Erasmo wakati mwamuzi msaidizi namba mbili ni Hamis Chang’walu. Mwamuzi wa mezani ni Israel Mujuni na Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Souleiman Waberi wa Djibouti.

Wakati huo huo, waamuzi kutoka Afrika Kusini ndiyo watakaochezesha mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Simba ya Tanzania na Clube Recreation Libolo ya Angola itakayofanyika Februari 17 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Waamuzi hao ni Daniel Volgraaff atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni Enock Molefe, Lindikhaya Bolo na Lwandile Mfiki. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Emmanuel Lesita kutoka Lesotho.

KIM AZIFUATA IVORY COAST, MOROCCO AFCON
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameondoka jana mchana (Januari 18 mwaka huu) kwa ndege ya South African Airways kwenda Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Ivory Coast na Morocco zinazoshiriki Fainali za 29 za Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazoanza kesho (Januari 19 mwaka huu) nchini humo.

KOCHA WA TAIFA STARS, KIM PAULSEN

Ivory Coast na Morocco ziko kundi moja na Tanzania (Taifa Stars) katika kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na inayoshika nafasi ya pili katika kundi hilo ambalo pia lina timu ya Gambia itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video