Wakati
kesho ndiyo mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uongozi
kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Bodi
ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) waombaji 36 wameshachukua na 18 tayari
wamesharejesha.
Idadi
hiyo ni kufikia leo mchana (Januari 17 mwaka huu). Pia Kamati ya
Uchaguzi ya TFF inasisitiza kuwa wanaorejesha fomu hizo kwa email
wanatakiwa kuzituma kwa Katibu Mkuu wa TFF kwa email ya [email protected] na si kwa email binafsi za wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi au maofisa wa TFF.
Waombaji
wanne walioongezeka katika orodha ni Blassy Kiondo kwa Kanda ya Katavi
na Rukwa, Eliud Mvella (Mbeya na Iringa), Geofrey Nyange (Morogoro na
Pwani), na Omari Abdulkadir kwa Kanda ya Dar es Salaam.
Orodha
kamili ya waombaji ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi na Omari Mussa
Nkwarulo (urais) wakati waombaji wa umakamu wa rais mpaka sasa ni
Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia.
Kwa
upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni
Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus
Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra
Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly
Mbise (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu
Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi
na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman
Kambi na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart
Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Nyange na Twahili Njoki
(Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala na Eliud Mvella (Iringa na Mbeya),
Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari
Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).
Kwa
upande wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu mpaka sasa ni
wawili tu. Yusuf Manji amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed
amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti.
SUPER WEEK TENA NDANI YA LIGI KUU YA VODACOM
Mzunguko
wa pili ya Ligi Kuu ya Vodacom utaanza Januari 26 mwaka huu huku kukiwa
na maombi ya televisheni ya SuperSport kuonesha mechi za Super Week
kama ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza.
Raundi
tano za awali katika ratiba ya mzunguko wa pili zinabaki kama zilivyo
wakati nyingine zilizobaki zitatolewa baada ya kuingiza mechi za Super
Week.
Wakati
huo huo, mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza unatarajia kuanza
Januari 26 mwaka huu. Ratiba ya ligi hiyo na tarehe rasmi ya kuanza
itatangazwa baada ya kupitiwa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) inayotarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki.
0 comments:
Post a Comment